Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam comrade Stanley Mkandawire leo amewaongoza viongozi wa Chama Mkoa huo kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ulipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) eneo la Terminal 1, ukitokea Kaskazini Unguja, Zanzibar jana.
Katika mapokezi hayo Comrade Mkandawire, alianbatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Comrade Juma Simba (Gadaffi), Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Mkoa.
Katika mbio za mwaka 2026, Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
Miradi hiyo imetajwa kuwa na thamani ya takribani Sh. bilioni 113 hadi 113.5
Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Stanley Mkandawile akishika Mwenge wa Uhuru akiongoza viongozi wa CCM mkoa huo kuupokea Mwenge, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Comrade Juma Simba (Gadaffi), akishika Mwenge huo. Chini ni viongozi walioambatana na Mkandawire.








No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇