Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Asha-Rose Migiro, leo tarehe 15 Aprili 2026 amefanya mazungumzo na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Lazarus Chakwera, katika Ofisi za CCM Lumumba, jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yalijikita katika hali ya kisiasa nchini pamoja na matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Mhe. Chakwera yupo nchini Tanzania kwa ziara maalum katika nafasi yake kama Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Mhe. Shirley Ayorkor Botchwey.







No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇