ALIYEKUWA Rais wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye kwa sasa anahudumu kama Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika katika Ukanda wa Pembe ya Afrika na Bahari Nyekundu, siku ya Ijumaa alikutana na Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir Mayardit, mjini Juba, alipokuwa akihitimisha ziara ya ngazi ya juu ya siku mbili nchini humo.
Katika ziara hiyo, alikutana na wadau muhimu wa kitaifa, kikanda na kimataifa katika jitihada za kuirejesha nchi katika hali ya utulivu. Pia alifanya mazungumzo na mawaziri mbalimbali muhimu ili kutathmini maendeleo na changamoto katika utekelezaji wa Mkataba wa Kufufua Amani wa Kutatua Mgogoro wa Sudan Kusini (R-ARCSS) uliosainiwa mwaka 2018.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇