Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Mhe. Mary Pius Chatanda (MCC) ameeleza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kwa kiasi kikubwa mageuzi ya kiuchumi kwa Wanawake.
Mwenyekiti Chatanda ameeleza kuwa Rais Samia ametoa kipaumbele kwa Wanawake katika kuwainua kiuchumi kwa kuandaa Mikopo ya Halmashauri ya Asilimia 10, kutenga Fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kutoa Mikopo kwa Wajasiriamali wadogo wadogo ikiwemo Wanawake pamoja kutenga Asilimia 30 ya Dhabuni za manunuzi Serikalini kwa Makampuni yanayoendeshwa na Wanawake ikiwa ni jitihada za kuhakikisha mwanamke anainuka kiuchumi.
Mwenyekiti Chatanda ameeleza hayo alipokuwa akifungua Kongamano la Wanawake nguvu ya Jamii ikiwa ni sehemu ya Shamra shamra kulekea Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2026, llililofanyika katika Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (EACLC), Ubungo Jijini Dar es Salaam lililoandaliwa na UWT Wilaya ya Ubungo Machi 06, 2026.
Mwenyekiti Chatanda amebainisha pia katika Sekta ya Siasa na kijamii Wanawake wamepata nafasi mbalimbali za Uongozi ikiwemo ongezeko la Wawakilishi Wanawake katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufikia asilimia 37.6 pamoja na Wanawake waliopata nafasi katika Baraza la Mawaziri kufikia asilimia 34, huku Wanawake wengine wakipata nafasi katika nafasi za Makatibu Wakuu wa Wizara.









No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇