Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Ndugu Halid Mwinyi (MNEC) amesaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Isimani na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu) William Lukuvi, nyumbani kwake Area D jijini Dodoma, leo.
Enzi za uhai, Lukuvi aliwahi kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi UVCCM ikiwemo kuwa Katibu wilaya za Masasi, Mtwara, Arusha na Dodoma, Ujumbe wa Baraza Kuu na Kamati ya Utekelezaji Taifa, Mkuu wa Idara ya Oganaizesheni, Katibu mkoa wa Dar wa Dar es Salaam na mwisho alikuwa Naibu Katibu Mkuu.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇