Na Bashir Nkoromo, Tegeta.
Maelfu ya Uzao Halisi na Watekeleza Sauti Halisi wa Kanisa Halisi la Muumba kutoka Mataifa mbalimbali, ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Kanisa hilo, utakaorindima, Lango la 12 Tamuzi 1 Majira Halisi (Jumapili, Aprili 5, 2026), Kao Kuu, Tegeta Namanga, Plot. 195, Jijini Dar es Salaam.
Baba Halisi amesema, mbali na Watekeleza Sauti Halisi na Uzao Halisi kutoka mataifa mbalimbali ndani na nje ya Tanzania viongozi na wageni mbalimbali wamealikwa kuhudhuria mkutano huo bila kubagua, kwa kuwa Kanisa Halisi ni la wote.
Amesema, pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utafanya maboresho mengi makubwa ikiwemo ya safu za uongozi katika ngazi mbalimbali ambapo baadhi ya nafasi ambazo hazikuwepo zitaongezwa.
Baba Halisi amesema, Mkutano huo utafanyika Sanjari na Ibada maalum, itakayotangulia, na amewakaribisha kwa upendo Uzao Halisi na Watekeleza Sauti kuhakikisha kila mmoja hakosi kuhudhuria kwenye Ibada na mkutano huo kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.
Your Ad Spot
Mar 30, 2026
Home
featuread
KIJAMII
KANISA HALISI HALIPOI, KUUNGURUMISHA MKUTANO MKUU JUMAPILI IJAYO, LANGO LA 12 TAMUZI 1MH, KAO KUU, JIJINI DAR ES SALAAM
KANISA HALISI HALIPOI, KUUNGURUMISHA MKUTANO MKUU JUMAPILI IJAYO, LANGO LA 12 TAMUZI 1MH, KAO KUU, JIJINI DAR ES SALAAM
Tags
featuread#
KIJAMII#
Share This
About CCM Blog
KIJAMII
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇