ILI kuwapa vijana na wananchi wengine uhuru zaidi wa kujifunza mafunzo ya, ufundi stadi popote walipo na kwa muda wao, Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imeanzisha mfumo uitwao VSOMO unaomwezesha mwanafunzi kujifunza maarifa yote ya ufundi stadi kwa kutumia simu ya mkononi, kufanya mtihani kwenye simu hadi mwisho wa mpango wa mafunzo ya nadharia.
Mfumo huo
umeelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Anthony Kasore alipokuwa akizungumza
na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Wizara ya Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo katika Mji Serikali Mtumba
jijini Dodoma Februari16, 2026, kuhusu mafanikio ya utekelezaji wa siku 100 wa ahadi
zilizotolewa na Rais Samia alipoapishwa Novemba 3, 2025.
“Baada ya hapo, atapangiwa kufanya mafunzo ya vitendo
kwenye chuo kimojawapo cha VETA. Hii inapunguza muda wa kukaa chuoni na
inaongeza matumizi bora ya simu za mkononi na muda wa mafunzo. Vilevile, mpango huu unawapa fursa watu walio mbali na
vyuo kupata mafunzo ya ufundi stadi,”amesema CPA Masore.
“VSOMO ilikuwa ikitekelezwa kwa ushirikiano wa VETA,
Airtel na Kampuni ya Magilla Tech. Hata hivyo, mwaka jana, VETA ilikabidhiwa
rasmi mfumo huu ambapo kwa sasa VSOMO inapatikana kupitia mitandao yote ya simu
iliyopo nchini. “
Ametaja stadi zipatazo ishirini (20) zinazotolewa kupitia
mfumo wa VSOMO, kuwa ni; Ufundi wa Pikipiki; Ufundi wa Umeme; Ufundi wa Aluminium na PVC; Umeme wa Magari;
Utandazaji na Ufungaji Mabomba; Utengenezaji wa Kompyuta; Upishi na Utoaji
Huduma ya Chakula (Catering); Uokaji Mikate na Upambaji; Usafi wa Majengo
Makubwa na Maeneo ya Umma; Maua na Upambaji kwenye Shughuli; Ujasiriamali; Utengenezaji
wa Simu za Mkononi; Ufungaji Mabomba Viwandani; Umeme wa Viwandani; Uungaji
Vyuma Viwandani na Urembo.
Mpaka sasa Takribani wanafunzi 533 wamemaliza kozi
mbalimbali kupitia mfumo huu wa VSOMO na kutunikiwa vyeti.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA, CPA Antony Masore.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa Idara ya Habari MAELEZO na VETA wakiwa katika mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, Kelvin Kanje akihitimisha mkutano huo.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA - 0754264203
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇