LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 5, 2026

NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA ASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 49 YA CCM MKOA WA MWANZA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM, Mheshimiwa Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika katika Jimbo la Sumve, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza, leo tarehe 05 Februari, 2026.


Maadhimisho hayo yalifanyika chini ya kauli mbiu isemayo “Tumechagua Umoja na Amani kwa Maendeleo ya Taifa letu.”

Akihutubia wananchi na wanachama wa CCM, Ndugu Mongella amesema Chama Cha Mapinduzi kinatimiza miaka 49 kikiwa kimejikita katika misingi ya Amani, Umoja na Mshikamano, ambayo imeendelea kuwa nguzo muhimu ya maendeleo na ustawi wa Taifa letu. 

“Amani ndiyo msingi wa maendeleo ya nchi yetu. Bila amani, hakuna maendeleo yanayoweza kupatikana,” alisema Mongella.

Aidha, amewapongeza Viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Mwanza kwa usimamizi madhubuti na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, akieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana ni matokeo ya uongozi thabiti wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi. 

Maadhimisho hayo yalihitimishwa kwa wito kwa Wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kuendelea kulinda Amani, Umoja na Mshikamano kwa maendeleo endelevu ya Taifa.

 “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.”




 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages