LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2026

MAWAZIRI, VIONGOZI WAELEZEA MBELE YA WANAHABARI KUHUSU ZIARA YA RAIS SAMIA ETHIOPIA, DUBAI

 


Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2026 kuhusu Ziara za Kikazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026 pamoja na Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026. 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahamoud Thabit Kombo akizungumza na Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2026 kuhusu mafanikio ya Ziara ya Kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026. Waziri Mhe. Balozi Kombo alielezea kwa kina ushiriki wa Tanzania katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika mkutano huo.

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Kundo Mathew akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu Ziara ya Kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026. Naibu Waziri Mhandisi Kundo alizungumzia kwa kina masuala mbalimbali yaliyojiri kwenye sekta ya maji pamoja na faida ambazo Tanzania imepata katika mkutano huo. 


Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Biashara ya Kimataifa na Diplomasia ya Uchumi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi John Ulanga akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu Ziara ya Kikazi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyofanya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026.  Mhe. Balozi John Ulanga alielezea fursa mbalimbali ambazo Tanzania imepata kupitia Uwekezaji wa Teknolojia ya Mawasiliano. 


Waandishi wa Vyombo mbalimbali vya Habari wakiwa kwenye Mkutano kuhusu Ziara za Kikazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026 pamoja na Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026.





Viongozi mbalimbali waliohudhuria Mkutano wa Waandishi wa Habari, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2026 kuhusu Ziara za Kikazi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alizofanya Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 12-15 Februari, 2026 pamoja na Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) tarehe 2-6 Februari, 2026. 






 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages