LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 29, 2026

WAZIRI MKUU KUSHUHUDIA WABUNGE WANAZI WA YANGA, SIMBA WAKIONESHANA UBABE AZANIA BUNGE BONANZA

Mashabiki wa Klabu za Simba na Yanga wametambiana kwamba wataoneshana ubabe katika mashindano ya Azania Bunge Bonanza 2026 litakalofanyika kwenye viwanja vya St Merlin Miyuji jijini Dodoma Jumamosi Januari 31, 2026.


Tambo hizo zimefanyika wakati wa mkutano na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa jijini Dodoma leo Januari 29, 2026 ambapo Benki ya Azania wadhamini wa bonanza hilo wamekabidhi vifaa vitakavyotumika kwa Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga. Vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa ni; jezi, suti za michezo, mipira na medali mbalimbali.

Mgeni rasmi katika bonanza hilo  litakalo changamshwa pia na wabunge mashabiki wa vilabu hivyo, anatarajia kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba. 

Michezo itakayo shindaniwa katika katika bonanza hilo litakaloanza kwa matembezi yatakayoongozwa na Waziri Mkuu, kutoka Chuo cha Mipango hadi St. Merlin ni; soka,netibali, wavu, mpira wa kikapu, mbio, kukimbia kwenye magunia, kukimbiza kuku , kula wali, kunywa soda, bao, drafti na mingineyo.

Bonanza hilo litashirikisha wabunge, watumishi wa bunge, watumishi wa Benki ya Azania na taasisi nyingine pamoja na wanamichezo mbalimbali.

Washindi watapatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo  medali na vikombe.

 Mwenyekiti wa Bunge Bonanza, Festo Sanga (aliyevaa kaunda suti katikati) akiwa na mashabiki wa Yanga na Simba.
Viongozi wa Benki ya Azania wakikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa Sanga.









 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages