LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 2, 2026

USAFIRI WA SGR KUREJEA KESHO JUMAMOSI

Serikali imetangaza usafiri wa treni ya mwendo kasi (SGR) utaanza kesho jioni.

Kauli hiyo imetolewa leo ljumaa Januari 2, 2025 na Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbalawa wakati akizungumza na wananchi wa Gulwe wilayani Mpwapwa.

Waziri Profesa Mbalawala ametaja sababu za kusimamishwa usafiri huo ni kufanya uhakiki wa miundombinu ya reli yote kwa baadhi ya maeneo waliyokuwa na mashaka.

Ametaja eneo la Kidete Wilaya ya Kilosa kwamba lilikuwa na changamoto kidogo kwenye tuta la reli ambako mafundi wanaendelea kukamilisha.
'Niwahakikishie Watanzania kuwa kesho jioni usafiri wa SGR utarejea kama kawaida bila shida na watu wetu watambue ni lazima tujiridhishe kazi ambayo tumefanya na kuona tuko salama," amesema. Profesa Mbalawala.

Waziri Mkuu Dk Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kuacha kusikiliza alichokiita propaganda za watu kuhusu usafiri wa treni ya mwendo kasi kwa kuwa unahusu maisha ya watu wengi.


 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages