LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 2, 2026

CHATANDA AWASIHI WATANZANIA KUILINDA,KUIDUMISHA AMANI



Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amewaasa Watanzania kudumisha Amani, Umoja na Ushirikiano wa kidugu baina yao kwa kuwa ndiyo nguvu inayoliunganishaTaifa la Tanzania.


Chatanda ameyasema hayo  Januari 01, 2026  alipohudhuria ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya 2026, kwenye Kanisa la KKKT Usharika wa Ndiuka Dayosisi ya Iringa, mkoani Iringa, na kuwasihi waumini na Watanzania kwa ujumla kuwa Amani ni Tunu ya kulindwa kwa nguvu zote na "tusiruhusu ama kukubali kushawishiwa kwa fedha kuivuruga Amani iliyopo Nchini."

Katika hatua nyingine Chatanda amewataka Wazazi kutowaacha watoto wajilee wenyewe kitendo ambacho hukosa maadili, Mila na Desturi, hivyo wazazi wawajibike katika kuwapeleka shule na kuwasimamia Malezi ya Watoto na kuhakikisha wanakuwa katika misingi ya kumcha Mungu ili wawe kwenye mazingira mazuri ya ukuaji.













 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages