NAFASI za kujiunga na mafunzo ya kujitolea Jeshi la KujengaTaifa (JKT), haziuzwi bali hutolewa bure kwa raia wa Jamhuri ya Muungano waTanzania wenye vigezo maalumu.
Tahadhari hiyo imetolewa kwa wananchi na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Brigedia Jenerali, Hassan Mabena alipokuwa akitangaza nafasi hizo mbele ya vyombo vya habari katika Makao Makuu ya JKT jijini Dodoma leo Januari 20, 2026.
"Msisitizo, nafasi hizi haziuzwi, nafasi hizi haziuzwi, kwa hiyo asije akatokea mtu yeyote akatumia fursa hii kwamba anaweza kumpatia mtanzania yeyote nafasi ya kujiunga na JKT kwa kuweza kumpatia kiasi cha pesa." Amesema Brigedia Jenerali Mabena.
"Kama nilivyosema kuwa kuna baadhi ya watu wanaitumia mitandao vibaya, waitumia kuweza kutapeli watu. Mtu anatuma meseji kwamba nafasi zile zimetangazwa, mimi nina uwezo wa kukupatia nafasi toa laki tatu, toa milioni moja, toa milioni moja na laki tano. Nafasi hizi haziuzwi bali hutolewa kwa vijana waliotimiza vigezo," amesisitiza Brigedia Jenerali Mabena.
Amesema kuwa nafasi zote hutolewa wilayani na mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na kwamba usajili utaanza rasmi Januari 26 hadi Februari 26, 2026 na watakaofanikiwa wanatakiwa kuanza kuripoti katika kambi za JKT kuanzia Februari 27 hadi Machi 4 mwaka huu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA-0754264203
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇