MKUU wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena akitangaza kwa niaba ya Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele nafasi za vijana kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo ambapo pamoja na mambo mengine vijana hao watapata mafunzo ya uzalendo wa Nchi katika mitandao. Usajili kwa vijana raia wa Tanzania Bara na Visiwani utaanza Januari 26 hadi Februari 26, 2026 na watatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT kuanzia Februari 27 hadi Machi 4 mwaka huu.
Nafasi hizo zimetangazwa mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya JKT jijini Dodoma leo Januari 20, 2026.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇