LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 16, 2026

JWTZ YATOA MSAADA KWA WANANCHI

 

.Mkuu wa shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania Brigedia Sijaona Muyala amewaongoza Maafisa na Askari wa Jeshi kutoa msaada kwenye jamii ya kitongoji Cha Lukenge kilichopo Kijiji Cha Kihangaiko kata ya Msata wilaya ya Bagamoyo Mkoa Pwani .

Msaada huo umetolewa kwa wananchi ikiwa ni zoezi la medani lijulikanalo kama EXERCISE MALIZA
Linalofanya na kuruti lenye lengo la kuimarisha mahusiano na wananchi wa eneo hilo.

Mkuu wa shule hiyo ya awali ya mafunzo ya kijeshi Brigedia Muyala amesema zoezi hilo la utoaji msaada kwa Jamii ni kuimalisha ushirikiano baina ya Jeshi na wananchi ikiwa pamoja na ulinzi na usalama kwa wananchi.

Brigedia Muyala amesisitiza kuwa Jwtz kitaendelea kutoa misaada ya kibinadamu  pindi inapohitajika katika eneo lao ili kudumisha umoja na ushirikiano mzuri ulipo katika eneo kwa JWTZ na wananchi .

Aidha mganga wa hospital ya shule ya mafunzo ya awali ya kijeshi RTS kihangaiko meja Edwin Mboya amesema timu ya madaktari na wahudumu ilitoa elimu  na tiba kwa wananchi 200 sambamba kupatiwa matibabu pamoja na uchunguzi  wa afya na tiba.

Mwenyekiti wa kitongoji Cha kihangaiko Shabani Mkomo alipongeza JWTZ kwa msaada walioutoa kwa wananchi ambao umekuwa na manufaa makubwa lakini pia wanashukuru kwa kuendelea kudumisha uhusiano ulipo baina ya wananchi na Jeshi Hilo.

Baadhi ya wananchi nao kibwana mtiko na stela losai wameshukuru msaada waliopatiwa.

Jeshi la wananchi wa Tanzania limeendelea kutoa misaada mbalimbali pamoja na huduma kwa Jamii ikiwa lengo ni kudumisha uhusiano  na ushirikiano Tangu  kuhasisi tarehe 1 September 1964.









 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages