Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) AntĂłnio Guterres, amesema Tanzania inaendelea kuwa mfano wa amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote.
Amesema hayo, jana alipokuwa akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambao uliwasilishwa na Mjumbe Maalum, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Kombo.
Katibu Mkuu Guterres alieleza kuwa kutambua sifa ya Tanzania kama nembo ya amani ilipimwa wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, na kupongeza uthabiti wa nchi katika kudumisha umoja na utulivu wa kitaifa.
Alisisitiza ni maslahi ya Umoja wa Mataifa kuiona Tanzania ikiendelea kubaki imara na kutumika kama mfano chanya.
Katibu Mkuu huyo pia alisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi, kwa lengo la kushughulikia mizizi ya matukio ya vurugu yaliyotokea siku hiyo ya Oktoba 29, 2025, na kuweka mikakati ya kuzuia kujirudia kwa matukio kama hayo.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇