LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 29, 2025

SERIKALI YATUMIA BILIONI 17 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA YA KINYWA NA MENO

Na Mwandishi Maalum, TDA, Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Afya imewekeza kiasi cha Sh. Bilioni 17 kwa kununua vifaa vinavyohitajika katika kuboresha utoaji wa huduma za kinywa na meno hapa nchini.

Yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akizungumza katika Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya kinywa na meno Tanzania (TDA), uliofanyika hivi karibuni, jijini Dodoma, akimuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe. 
Alisema, kupitia uwekezaji huo wa vifaa tiba kwa ajili ya huduma za meno na uwepo wa madaktari bingwa waliowafikia wananchi kupitia huduma za mkoba zimesaidia wananchi kuepukana na adha ya kupoteza meno kwa kiasi kikubwa au kupata madhara zaidi

“ Hatua hii imeongeza ubora wa huduma na kuwawezesha madaktari bingwa kuwafikia wananchi kupitia huduma za mkoba, jambo ambalo limechangia kupunguza hatari ya kung’olewa meno au kupata madhara makubwa ya kiafya,” amesema Dkt. Makuwani.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Afya Dkt. Baraka Nzobo amewataka wananchi kujitokeza kwenye huduma mbalimbali zanazotolewa na mabingwa wa Afya na meno ili kutimiza dhana ya Wizara ya Afya ya kuondoa tatizo la mapengo au kibogoyo kwa kila mwananchi.

“Nawaomba wananchi wajitokeze kutumia huduma zetu za kitaalam , ili kutimiza dhamira ya Wizara ya Afya ya kuhakikisha kila Mtanzania anaepukana na tatizo la mapengo au kibogoyo maana kumekuwa na dhana mzee lazima ameng'oa meno mawili au matatu jambo ambalo sio kweli,” amesema Dkt. Nzobo.

Maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni 'Kuwezesha Ubunifu Wa Kiteknolojia Kukuza Afya Ya Kinywa Na Meno Tanzania' hufanyika kwa wiki nzima ambapo licha ya kufunguliwa kwenye mkoa mmoja unaochaguliwa, bado wananchi wananufaika nchi nzima kwa kukutana na madaktari bingwa wa afya ya kinywa na meno na kupatiwa matibabu.

Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akizungumza wakati akifungua rasmi  Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.
Rais wa Chama Cha Wataalam wa Afya ya Kinywa na Meno (TDA, Dk. Gema Berege akizungumza wakati wa Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Kinywa na Meno kutoka Wizara ya Afya Dkt. Baraka Nzobo akizungumjza wakati wa Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni. 

Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akimkabidhi Cheti cha Ushiriki, Mkurgenzi wa Dema & Omega Dental Dk. Jackson Mboya, wakati akifungua rasmi  Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni. 

Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akimkabidhi Cheti cha Ushiriki, Dk. Erick Sylivester wa Kampuni ya dawa za meno ya Whitedent, baada ya kufungua rasmi  Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.

Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akimkabidhi Cheti cha Ushiriki, Mratibu wa Afya ya Kinywa na Meno Kigamboni Mc Dk. Iddi Khery, baada ya kufungua rasmi  Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.

Mtoto mmoja wa Shule ya Msingi Dodoma Viziwi iliopo Kisasa mjini Dodoma, .akitoa elimu ya afya ya kinywa na meno  kwa wanafunzi wenzake, wakati TDA walipofika kutoa elimu ya afya ya kinywa na meno katika shule hiyo hivi karibuni.

Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akibadilishana mawazo na rais wa TDA Dk. Gema Berege (kushoto) alipowasili kwenye Kongamano na mkutano huo.
Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwa ajili ya ufunguzi rasmi  wa Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Idara ya Afya uzazi, Mama na Mtoto Dk. Ahmad Makuwani (wa pili kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa Programu wa Shirika lisilo la Kiserikali (NGo), linalotayarisha maonyesho ya Kibiashara ya Afya ya Kinywa na Meno la Dental Expo, Dk. Azama Kassanga, kwenye banda la NGo hiyo, baada ya kufungua rasmi Kongamano la 40 la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa Wataalam wa Afya ya Kinywa na meno Tanzania (TDA) uliofanyika Jijini Dodoma hivi karibuni. Zifuatazo ni matukio mbalimbai yaliyojiri karika tukio hilo.👇👇

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages