Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndugu John Mongella kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro leo tarehe 16 Desemba, 2025, amejumuika na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, pamoja na wananchi, katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama, yaliyofanyika Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma.
Akiwasilisha salamu za Katibu Mkuu wa CCM, katika shughuli hiyo iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Ndugu Mongella alisema kuwa Mhe. Jenista alikuwa kada na mwanachama mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi katika kipindi chote cha uhai wake, akiaminiwa kuwatumikia wanachama na wananchi, kupitia dhamana mbalimbali za uongozi ndani ya Chama na Serikali, kwa uadilifu na unyenyekevu mkubwa.






No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇