LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 16, 2025

DKT NCHIMBI AONGOZA MAZIKO YA MAREHEMU JENISTA MHAGAMA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, leo Desemba 16, 2025 ameongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Marehemu Jenista Mhagama, yaliyofanyika Kijiji cha Ruanda, Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.

Akizungumza mara baada ya mazishi, Dkt. Nchimbi amesema Taifa limepoteza kiongozi wa mfano aliyewatumikia wananchi kwa dhati, unyenyekevu na kujitoa bila kuchoka. Ameeleza kuwa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na wananchi kwa ujumla wamepoteza nguzo muhimu ambayo mchango wake utaendelea kukumbukwa kwa vizazi vijavyo.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa Serikali na CCM vitaendelea kuenzi maono na mchango wa marehemu kwa kusimamia uongozi unaoweka wananchi wa hali ya chini kuwa kipaumbele cha kila siku.

Aidha, amewasilisha salamu za pole na shukrani kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa familia, wananchi wa Ruvuma na viongozi wa Kanisa waliomshika marehemu katika safari ya mwisho.








 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages