LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2025

MKAZI WA BOKO, SHABANI KALOVA ARATIBU DUA ILIYOFANYIKA LEO KUMUINUA RAIS SAMIA 2026

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Mwananchi Shabani Kalova leo Jumatatu Disemba 29, 2025 ameratibu dua ya kumuinua Rais wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, kumuombea kwa Muumba wa wote,  yote na vyote amlinde na shari zote na kumjalia kila la heri mwaka 2026.


Dua hiyo iliongozwa na Sheikh Rashid Ally Farahani wa Masjid Hakhi katika eneo la Chasimba, Boko, Dar es Salaam, akiwa na wana madrasa zaidi ya 20 na kufanyika kwa zaidi ya saa tatu kuanzia saa nne asubuhi.


"Ee Mwenyezi Mungu tunakuomba umjaalie Rais wetu Samia Suluhu Hassan, afya njema, umjaalie, hekima na busara, aendelee kutuongoza vema.


Ee Mwenyezi Mungu mlinde na shari na mabaya yote, fikra za wabaya wote wenye nia ovu juu yake uzigeuze nia hizo kuwa njema, tunapongia mwaka mwingie (2026) Rais wetu asijikwae popote.


Tunakuomba kwa unyenyekevu ulizidi kulilinda taifa letu la Tanzania liendelee kuwa la amani na utulivu, maana taifa hili ndiyo letu, likikosa amani hatuna kwa kukimbilia", akaomba Sheikh Farahani baada ya kisomo hicho cha dua.


Kisha Mratibu wa hafla dua hiyo Shaban Kalova akazungumza, ikiwemo kwa nini aliamua kuratibu hafla hiyo. msikilize

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages