𝘼𝙨𝙚𝙢𝙖 𝘾𝘾𝙈 𝙞𝙣𝙖 𝙬𝙖𝙟𝙞𝙗𝙪 𝙬𝙖 𝙠𝙪𝙛𝙪𝙖𝙩𝙞𝙡𝙞𝙖 𝙪𝙩𝙚𝙠𝙚𝙡𝙚𝙯𝙖𝙟𝙞 𝙬𝙖 𝙞𝙡𝙖𝙣𝙞 𝙮𝙖𝙠𝙚 𝙠𝙬𝙖𝙠𝙪𝙬𝙖 𝙨𝙚𝙧𝙞𝙠𝙖𝙡𝙞 𝙞𝙣𝙖𝙩𝙤𝙠𝙖𝙣𝙖 𝙣𝙖 𝙘𝙝𝙖𝙢𝙖 𝙝𝙞𝙘𝙝𝙤.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. 𝗞𝗲𝗻𝗮𝗻𝗶 𝗞𝗶𝗵𝗼𝗻𝗴𝗼𝘀𝗶 amewataka watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia wananchi kwa kutanguliza utu na muda.
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa chama na jumuiya wa mkoa wa Dar es salaam, Mwenezi Kenani amesema kuwa wapo baadhi ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamika kuwa kwanini viongozi wa chama wamekuwa wakifuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ambapo ameeleza kuwa kitendo hicho ni kudhiirisha kuwa watumishi hao hawapo tayari kutekeleza majukumu yao kwa ukamilifu na kusema kufanya hivyo ni kuikosea heshima serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotokana na CCM na kuongozwa na Mwenyekiti na Rais Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.
Mwenezi Kenani ametuma ujumbe kwa baadhi ya watumishi hao akisema kuwa CCM hiataacha kufuatilia kila hatua katika utoaji hudumu wao kwa wananchi na utekelezaji wa miradi kwakuwa inayotekelezwa ni ilani ya uchaguzi ya CCM waliyoinadi.
"kuna baadhi ya watumishi wa umma wanasema chama kinawafatafata, waambieni tuna wajibu wa kuwafata kwakuwa ilani inayotekelezwa ni yetu na tutawafata kila wakati kuhakikisha wanafanya kazi iliyokusudiwa na Rais Mhe. Dkt. Samia"
"Ikiletwa fedha ya kituo cha afya basi chama kitakuja kukagua matumizi sahihi ya fedha hizo, hatutaacha kufanya hivyo kwakuwa watumishi wazembe ndiyi wenye kusababisha CCM ionekane haifanyi kazi"

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇