LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 19, 2025

TIDO MHANDO NA BAKARI MACHUMU WAULA IKULU

Tido Mhando  na Bakari Machumu wameteuliwa Kuongoza Kitengo cha Habari na Mawasiliano Ikulu, na Lazaro Nyalandu kuwa Balozi.

Hiyo ni baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufanya uteuzi mpya wa viongozi watakaosimamia maeneo muhimu ya mawasiliano na diplomasia.

Katika uteuzi huo:

 1. Bw. Tido Mhando ameteuliwa kuwa Mshauri wa Rais wa Habari na Mawasiliano, nafasi inayomrejesha katika mstari wa mbele wa kusimamia mikakati ya mawasiliano ya juu ya serikali.

 2. Bw. Bakari Steven Machumu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, akichukua nafasi ya Bi. Sharifa Bakari Nyanga, ambaye amepangiwa majukumu mengine ya kiuongozi.

 Machumu, anayefahamika kwa uongozi imara katika vyombo vya habari, anatarajiwa kuleta msukumo mpya katika usimamizi wa taarifa za serikali.

 3. Bw. Lazaro Samuel Nyalandu ameteuliwa kuwa Balozi, hatua inayomrejesha katika majukumu ya kidiplomasia baada ya safari ndefu katika uongozi wa umma.

Taarifa hii imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses Kusiluka, ikibainisha kuimarishwa kwa mifumo ya mawasiliano na diplomasia nchini.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages