Ni ngumu sana kutawala moyo wa mwanamke, hakuna mwanaume ambaye yupo salama kwenye hisia za mwanamke.
Mwanamke ataweza kukuacha kwasababu huna kazi, atakuacha kwasababu upo busy, na anaweza kukuacha pia kwasababu unampenda sana au kwasababu umekamilika sana na humpi vurugu au hekaheka.
Utampenda, utampatia maisha mazuri, utamjali, na bado atakuacha.
Huwezi kumzuia mwanamke asiekupenda abaki na wewe, atakuacha pia hata kama umekamilika kwa kila kitu.
Usiwe mwema sana kwa mwanamke wala kueleweka sana, kuishi na jinsia ya kike inahitaji akili zaidi kuliko hisia.
Wakati mwingine Wanawake wanapenda sana hekaheka za ugomvi na mabishano, wanapenda kulia na kuvumilia, anapenda ashindane na wenzake, wakati mwingine mwanamke anapenda ajihisi yupo kwenye mashindano na mwanamke mwingine.
Vurugu na mwanamke kwenye mahusiano sio jambo la hiari bali ni jambo la lazima, bila vurugu atatafuta sehemu nyingine itakayompa vurugu na hekaheka za kuvumilia.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇