Aliyekuwa Spika, Dkt. Tulia Ackson akila kiapo cha utiifu cha ubunge katika uapisho wa wabunge kwenye Ukumbi wa Bunge jijini Dar es Salaam Novemba 11, 2025.
Dkt. Tulia alijitoa kwenye kinyang'anyiro cha kuomba kuwania Uspika kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwaacha Mbunge wa Ilala na aliyekuwa Naibu Spika, Mussa Azzan Zungu na Stephen Masele.
Zungu aliibuka mshindi ndani ya CCM na baadaye kugombea nafasi hiyo na wagombea wengine watano kutoka vyama vya upinzani.
Zungu ameibuka kuwa Spika wa Bunge baada ya kuwabwaga wapinzani kwa kupata jumla ya kura 378 na kuwaachia kura mbili wapinzani.
Dkt. Tulia akipokea nyaraka za kufanyia kazi.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇