LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 2, 2025

DKT. SAMIA USIOGOPE MUNGU ATAKULINDA, ATAKUPA TENA KWA MIAKA 5 UONGOZE TAIFA LETU - MAKONDA

Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda, amemtoa hofu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia CCM, Rais  Dkt. Samia Suluju Hassan kwamba asiogope Mungu amembariki, atamlinda na  atampatia tena uongozi wa Nchi kwa miaka mingine mitano,kwani ameonesha ujasiri wa kuiongoza nchi katika vipindi vigumu.


Makonda ameyasema hayo alipokuwa akijinadi yeye katika mkutano huo wa kampeni ambapo pia alimuombea kura pamoja na madiwani wa chama hicho katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi za CCM kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 2, 2025.


."..Yapo maneno ya kukukatisha tamaa na kukuvunja moyo, nakuhakikishia umekaa kwenye kiti cha Urais kwa mapenzi ya Mungu na Mungu atakupa tena kwa miaka 5 kuendelea kuongoza Taifa letu la Tanzania.."


"..Nenda ukaifanye kazi na usiogoe, nimeifurahi sana kuona unazunguka mwenyewe na unatafuta kura wewe mwenyewe na huna Godfather, Godfather wako mi wapiga kura ambao ni Watanzania na wameonesha utayari wao kutiki kwako,"amesema Makonda huku akishangiliwa na wananchi.




Wananchi wakiwa wamefurika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kumsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa anajinadi yeye , wabunge na madiwani wa chama hicho kwa kuwaomba watanzania kuipigia CCM kura Oktoba 29, 2025.

Baadhi ya wazee wa kimila wakiwa katika mkutano huo.








 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages