Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mratibu wa Kampeni kwa mikoa ya Kanda ya Kati Ndugu. Balozi Dkt. Bashiru Ally, amesema Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 ni Rais aliyefanya kazi kubwa ya katika demokrasia ya kuinua uchumi wa Tanzania na kuleta maendeleo endelevu kwa kila Mtanzania.
Dkt. Bashiru ameyasema hayo wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Mwanza na maeneo ya karibu katika ufungaji wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kupitia CCM , leo tarehe 28 Oktoba 2025.
Pamoja na hayo, Balozi Dkt. Bashiru amegusia Tuzo mbalimbali alizopewa Mgombea Urais Dkt. Samia kutokana na kutambulika na kuthaminika kwa kazi kubwa anayoifanya katika kuliongoza vema Taifa la Tanzania kwa misingi ya falsafa yake ya Uongozi ya 4R.


No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇