Na Richard Mwaikenda, Pangani
Baadhi ya wafugaji wa jamii ya wamang'ati wakionesha furaha yao na kuahidi kumpigia kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk.Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni za CCM Pangani Mjini mkoani Tanga Septemba 29, 2025.
Akihutubia katika mkutano huo Dkt. Samia amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza tena nchi kwa kumpigia kura Oktoba 29, 2025, Serikali itaendelea na utoaji wa ruzuku katika chanjo ya mifugo, ujenzi wa majosho na mabwawa ya kunyweshea, lakini pia wataendelea kutenga maeneo ya kufugia ili kupunguza migogoro na wakulima,
Pia ameahidi kulifanyia kazi ombi la kujenga Bandari ya Mifugo Pangani.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇