LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 10, 2025

MATOKEO YA UTAFITI: UONGOZI IMARA CCM WAPOROMOSHA VYAMA VYA UPINZANI Z'BAR

Mwinyi, Dimwa wasifiwa kwa busara na utulivu


Na Dkt Dismas Lyassa


Katika utafiti uliofanyika visiwani Zanzibar, imebainika kuwa uongozi wa Rais Dkt. Hussein Mwinyi, kwa kushirikiana kwa karibu na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Mohammed Said Mohammed Dimwa, umeleta mabadiliko makubwa ya kisiasa ambayo kwa kiasi kikubwa yameyumbisha vyama vya upinzani na kuyafanya yapoteze mvuto na nguvu ya ushawishi kwa wananchi. 

 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed (DIMWA), Katibu wa Kamati Maalum ya Nec, Idara ya Itikadi, Mafunzo na Uenezi (CCM) Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis pamoja na Katibu wa Kamati Maalum ya Nec, Idara ya Organaizesheni (CCM) Zanzibar Ndg. Omar Ibrahim Kilupi wamefanya ziara ya kumtembelea na kumjulia hali Mbunge Mstaafu (CUF) Jimbo la Malindi Maalim. Muhammad Ibrahim Sanya nyumbani kwake Mbweni, mojawapo ya vitendo ambavyo vilionekana kujali utu.


1. Utendaji wa Dkt. Hussein Mwinyi: Uongozi wa Vitendo, Sera za Kivitendo

Utafit huo uliofanywa na taasisi ya Tuwainue Foundation chini ya mwandishi wa habari na Mtaaam wa Uongozi, Dkt Dismas Lyassa, wananchi wengi walieleza kuwa tangu Dkt. Mwinyi aingie madarakani, amekuwa kiongozi anayetekeleza ahadi kwa ufanisi na kwa kasi ya kuridhisha. Amejikita katika:

Kurejesha imani ya wananchi kwa serikali kwa kupambana na rushwa na ubadhirifu

Kukuza uchumi kupitia uwekezaji na utalii

Kuboreshwa kwa huduma za jamii kama afya na elimu

Hali hii imefanya wananchi wengi, hata waliokuwa wafuasi wa vyama vya upinzani, kuhamasika zaidi kuiunga mkono CCM kwa sababu maendeleo yanaonekana na kunufaisha watu wa kada zote.

2. Dimwa: Mwanasiasa Shupavu, Anayeunganisha Chama na Wananchi

Moja ya majibu yaliyojitokeza mara kwa mara kutoka kwa washiriki wa utafiti ni kwamba Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Mohammed Said Mohammed Dimwa, ameleta sura mpya katika siasa za chama. Wananchi walimtaja kama:

Kiongozi shupavu, mwenye ukaribu na wananchi wa kawaida

Msemaji makini na mwenye hoja zenye mvuto

Mwana-CCM anayesimamia nidhamu ya chama huku akihamasisha mageuzi na uwajibikaji

Kwa kauli za watu waliowahi kuhojiwa:
“Dimwa anatufanya tuone CCM ni chama chetu. Siyo tena chama cha wakubwa tu.”

Ni wazi kuwa mchango wake umeongeza mvuto wa CCM miongoni mwa makundi ya vijana, wanawake, na hata baadhi ya waliokuwa wapinzani.

3. Vyama vya Upinzani Zanzibar: Sauti Zimezimika

Utafiti umeonyesha kuwa kutokana na utendaji wa viongozi hao wawili, vyama vya upinzani Zanzibar vimepoteza mwelekeo, nguvu ya kuhamasisha, na mvuto kwa wananchi. Washiriki wengi wa utafiti walisema:

Vyama vya upinzani havina tena sera mbadala zenye mashiko

Viongozi wake hawasikiki tena hadharani kama ilivyokuwa awali

Wanachama wengi wamehamia CCM au wamejiondoa kwenye siasa kabisa

Kauli nyingine iliyorudiwa mara kadhaa katika utafiti ni:
“Zamani upinzani ulikuwa na nguvu Zanzibar. Sasa hivi hata ukiuliza viongozi wake wakuu ni akina nani, wengi hawajui.”

Kutokana na ushahidi wa wazi kutoka kwa wananchi na uchambuzi wa mwenendo wa kisiasa visiwani, ni dhahiri kuwa mseto wa uongozi makini wa Dkt. Mwinyi na Dimwa umeibomoa kwa kiasi kikubwa ngome ya upinzani Zanzibar. Hili limeifanya CCM kuimarika zaidi kama chama chenye mwelekeo, kinachoaminika, na chenye uwezo wa kuongoza serikali na jamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages