Na CCM Blog, Dar es Salaam
Katika kuhakikisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inafanya kazi kwa ubora wa kiwango cha juu Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeiwezesha Mamlaka hiyo kununua mitambo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara.
Akizungumza katika Mikutano na Wahariri wa Habari, jijini Dar es Salaam leo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dk. Fedelis Mahumiko, amesema kufuatia hatua hiyo ya serikali, ununuzi wa mitambo ya uchunguzi wa kimaabara umeongezeka kwa asilimia 23.6, kutoka Sh. Bilioni 13.6 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 hadi 2021/2022 hadi kufikia thamani ya jumla ya Sh. Bilioni 17.8 kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 kwa kuongeza mitambo mikubwa 16 na midogo 274.
Amesema ununuzi wa mitambo hiyo umeendelea kuimarisha uchunguzi wa kimaabara na kuendelea kutoa huduma bora za uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.
"Utoaji Huduma za Kimaabara katika Viwango vya Kimataifa Katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita pia Mamlaka imefanikiwa kuendelea kutoa huduma za Uchunguzi wa Kimaabara na matokeo yake kukubalika katika ngazi na
Viwango vya Kitaifa na Kimataifa.
Kukubalika huko kwa matokeo ya uchunguzi kunatokana na Mamlaka kutekeleza mifumo miwili ya ubora na umahiri ya kimataifa, ambayo ni Ithibati ya Mifumo ya Usimamizi wa Ubora (ISO 9001:2015) ya uendeshaji wa shughuli za Mamlaka uliyohuishwa kwa mara nne mfululizo na mfumo wa Ithibati katika Umahiri wa uchunguzi wa kimaabara (ISO 17025:2027).
Katika kipindi cha miaka mine cha Serikali ya awamu ya sita pekee, Mamlaka imefanikiwa kupata ithibati katika Umahiri wa uchunguzi wa kimaabara (ISO 17025:2027) kwenye
maabara zake sita ambazo ni: Maabara ya Vinasaba vya Binadamu, Mikrobiologia, Sayansi Jinai Toksikologia, Mazingira, na Kanda ya Ziwa – Mwanza ikiwemo maabara ya Chakula.
Mafanikio haya ni makubwa na muhimu kwa kuwa, kunaifanya Mamlaka kukidhi matakwa ya Kisheria na mifumo ya Ubora katika ngazi ya kitaifa na kimataifa." Amesema Mtendaji Mkuu Dk. Fedelis Mahumiko.
Kuhusu mchango kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali, Dk. Fedelis Mahumiko, amesema, Mamlaka imeendelea kuhakikisha inachangia mfuko huo ikiwa ni sehemu yake kuchagiza maendeleo ya Nchi.
Amesema, katika kipindi cha miaka minne, Mamlaka imefanikiwa kuchangia kwenye Mfuko huo jumla ya Sh. 3,999,375,100.00 kupitia
maduhuli iliyoyakusanya.
Dk. Fedelis Mahumiko, amesema pia katika kuendelea Kuimarisha Usimamizi wa shughuli za Mamlaka Katika kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Awamu ya Sita, kwa miaka Minne mfululizo (2021/2022 hadi 2024/2025) imepata hati safi za ukaguzi wa Hesabu zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
"Aidha, kutokana na utendaji mzuri wa Mamlaka inategemea kuendelea kupata hati safi kwa kuendelea kuboresha na kuongeza ufanisi katika utendaji wake wa kazi.", amesema Dk. Fedelis Mahumiko.
Afisa Habari wa Ofisi ya Msajili wa hazina Alex Malanga akiongoza kikao hicho.Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelis Mahumiko, akizungumza wakati akihitimisha kikao hicho. Tafadhali soma wasilisho kamili kama alivyoliwasilisha kwenye kikao hicho👇



















No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇