Jun 2, 2025

UZINDUZI WA ALBAMU YA CHANZO HALISI AMEKUJA WANOGESHA IBADA YA KANISA HALISI LA MUUMBA

Ibada iliyofanyika leo Jumapili Juni Mosi, 2025 katika Knaisa Halisi la Muumba lenye Makao yake Makuu, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, ilikuwa ya aina yake baada ya kuambatana na uzinduzi rasmi wa Albamu ya Chanzo Halisi Amekuja,  uliofanywa na kundi la Waimbaji wa Kanisa hilo.

Katika uzinduzi huo uliofanyika mwinshoni mwa Ibada, baada ya Waimbaji kuzindua kwa kuimba nyimbo zote 12 zilizomo kwenye Albamu hiyo, baadaye flash zenye nyimbo hizo zilinadiwa na kukusanya zaidi ya sh. milioni 25, ikiwemo iliyonunuliwa kwa ajili ya Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi BABA HALISI, ambayo Uzao na Watekeleza Sauti waliipia zaidi ya Sh. milioni 10.

Flash nyingine zilinunuliwa na kukabidhiwa viongozi Waandamizi wa Kanisa hilo akiwemo Amani Halisi ambaye aliendesha Ibada hiyo. 

Mama Halisi akizungumza kutoa salam maalum wakati wa Ibada hiyo. Wapili kulia ni Mnara Mmoja Halisi na watatu ni Dada Udhihirisho Halisi.
Amani Halisi akiongoza Ibada hiyo.
Mama Halisi akipokea Shukurani wakati wa Ibada hiyo, akiwa na Mnara Mmoja Halisi na Dada Udhihirisho Halisi.
Viongozi waandamizi wa Kanisa Halisi wakipokea shukurani wakati wa Ibada hiyo.
Amani Halisi akinyunyiza dau safi nyeupe kuoeleka Ibada hiyo Mataifa yote.
Kisha akafanya shukurani kurasimisha kwa Muumba Damu hiyo safi nyeupe.
Kisha ukaimwa wimbo kusindikiza shukurani iliyofanywa na Amani Halisi.
Mama Halisi akizungumza kutoa salam maalum wakati wa Ibada hiyo. Wapili kulia ni Mnara Mmoja Halisi na watatu ni Dada Udhihirisho Halisi.
Kisha Mnara Mmoja Halisi pia akazungumza sanjari na Salam hizo maalum alizotoa Mama Halisi.
Mnara mmoja Halisi akainua shukurani kwa Muumba baada ya kuzungumza.
Dk. Uelewa na viongozi waandamizi wenzake wa Kanisa hilo wakipokea shukurani hiyo.
Uzao na Watekeleza sauti wakipokea shukurani hiyo iliyoinuliwa na Mnara Mmoja Halisi.
Mnara Mmoja Halisi akitoa Matunda ya Shukurani.
Kisha Mnara Mmoja Halisi akaimba wimbo maalum.
Wimbo ulipolea yeye, Mama Halisi na Dada Udhihirisho wakacheza.
Wakaendelea kucheza kwa shangwe.
Dk. Uelewa Halisi akitoa matunda.
Uzao na Watekeleza Sauti pia wakacheza wimbo huo maalum wa Mnara Mmoja Halisi.
Shangwe na hoihoi za Kumtukuza Muumba zikazidi.
Mwimbaji akikoleza rap kwenye wimbo huo kuzindisha amsha-amsha.
Mpapasa Kinanda akikoleza wimbo huo.
Uzao wakazindi kuserebuka kumtukuza Muumba.
Amani Halisi akaendelea na Ibada hiyo.
Waimbaji wakicheza moja ya nyimbo zilizpo kwenye Abamu ya Chanzo Halisi amekuja walipopanda jukwaani kuzindua Albabu hiyo.
Dada Udhihirisho akiimba kwa nguvu zake zote  wimbo wa Chanzo Halisi amekuja, wakati albamu ikizinduliwa kwa kuimbwa nyimbo zote 12 zilizopmo kwenye Albamu hiyo.
Baadhi ya Watekeleza Sauti wakimshangilia Dada Udhihirisho wakati akiimba.
Uelewa wa Sauti akiongoza kuimba wakati wa uzinduzi wa Albamu hiyo,
Uelewa wa Sauti akiongoza kucheza na kuimba wakati wa uzinduzi wa Albamu hiyo,
Kisha ikasomwa risala kuhusu uzinduzi wa Albamu hiyo.
Uzao na watekeleza sauti wkaketi sasa kusikiliza kinachofuata.
Flash zenye nyimbo zikaletwa kwa Amani Halisi kisha akazifanyia shukurani.
Uelewa wa Sauti akinadi Flash hizo.
Baada ya kunadi akamkadhi Amani Halisi Flashi yake iliyolipiwa na Uzao na Watekeleza Sauti kwa sh. milioni 5.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages