Anaandika Emmanuel J. Shilatu
Utasikia "Mama anaupiga, Mitano tena kwa Mama, hadi kufikia hatua ya kila kitu kizuri kuonekana amefanya Mama nikiwa na Maana ya Mama Samia.
Wapo wanaosema anayoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ni sehemu ya kutimiza wajibu wake, hapaswi kupongezwa; Wengine wanasema anayoyafanya hayastahili kutangazwa na wala hastahili kusifiwa kwani tutamfanya aanze kuharibu; ila wapo wengine wanaona anastahili kutiwa moyo na kupongezwa.
Kila Mtu ama kundi la Watu lina mitazamo yake. Nimekusanya mitazamo yote na hatimaye nikajiuliza, Je ni sahihi kumsifia Rais Samia kwa yale anayoyafanya?
Nasema, ni sahihi kabisa kwa Watanzania kumsifia mtangulizi wake Dk. John Magufuli kutokana na sababu zifuatazo, twende sawa hapa;-
Mosi; Watanzania wanayo haki ya Kikatiba kwa mujibu wa Ibara 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inatoa uhuru wa kutoa maoni na mawazo. Kumsifia Rais Samia ni sehemu ya Wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba ya kutoa maoni na mawazo yao.
Pili; Watanzania wana haki yao kabisa kumsifia Rais Samia anayetimiza wajibu wake wa kutekeleza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu 2020 - 2025 inayotokana na ilani ya uchaguzi. Kusema utafanya ni kitu kingine, kutekeleza ahadi yako ni jambo lingine. Kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza ahadi zake ni sehemu ya kuonyesha, kukubali na kumuunga mkono kile anachokifanya.
Tatu; Wananchi wana haki ya kujivunia kumpongeza Rais Samia ambaye anaiongoza vyema Serikali yake inayotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukusanya kodi ipasavyo. Kodi hizo hizo zinazokusanywa ndizo hizo hizo zinazoenda kutuletea maendeleo Watanzania mfano ukamilishwaji wa miradi ya maendeleo ya kimkakati, ujenzi wa miradi ya maendeleo kwenye sekta za afya, elimu, maji nk.
Nne; Watanzania wanayo haki ya kujivunia kumpongeza Rais Samia kwa kuhakikisha anatumia vyema kodi inayokusanywa kwa kuwaletea maendeleo Wananchi. Mathalani ununuzi wa ndege, vivuko, ujenzi wa reli ya kisasa ya standard gauge, ujenzi wa miundombinu ya madaraja, barabara, flyovers yote ni matunda ya matumizi sahihi na makini ya kodi zinazokusanywa. Sote ni mashuhuda miradi yote hiyo ameikamilisha ipasavyo na imeanza kutumika.
Narudia tena kusema, kumsifia Rais Samia kwa mema anayoyafanya kwa Taifa ni sahihi kabisa, ni sehemu ya uzalendo wenyewe wa Mtanzania kwa Taifa lako.
Kama tunaona barabara zinajengwa, madaraja yanajengwa, vivuko vipya vya kisasa vinazinduliwa, ndege mpya zinanunuliwa, reli ya kisasa imekamilika na nyingine inajengwa, flyovers zinajengwa, elimu bure inatolewa, dawa hospitalini zipo, umeme umesambazwa mpaka vijijini, hakika ametekeleza kwa vitendo ilani ya uchaguzi. Kwanini Watanzania tusijivunie kumpongeza Rais Samia?
Nahitimisha andiko hili kwa kumpongeza Rais Samia kwa uzalendo wake kwa Taifa, utekelezaji wa ilani ya uchaguzi inayowaletea maendeleo Watanzania na kuendesha nchi vyema kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Najivunia kumsifia Rais Samia. Tuendelee kumpongeza na kumtia moyo kwa mema yake anayoyafanya kwa Taifa na kwa Watanzania, historia na vizazi vitamkumbuka kama ambavyo Leo hii tunamkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere, Hayati Dk. John Pombe Magufuli na wengineo wengi.
Shilatu E.J
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇