Na Bashir Nkoromo, CCM's Blog
Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu amesema, Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH) katika mikakati yake ya kuendelea kuboresha taasisi na mashirika ya umma kuwa imara kiuchumi itachukua pia baadhi ya maelekezo kutoka kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2025/30.
"Katika mikakati yetu ya kuimarisha mashirika na tasisi za umma kuna baadhi ya mambo tutaçhukua kutoka katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ili kurandana na maelekezo ya Chama kilichounda serikali", alisema Mchechu kujibu swali la mwandishi wa habari hii, aliyetaka kujua kama anaionaje Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025/30 iliyozinduliwa wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Mei Mei 30 mjini Dodoma.
Mwandishi wetu alipata fursa ya kuuliza swali hilo, baada ya Mchechu kumaliza Kikao kazi na Wahariri wa Habari kilichofanyika Jumatatu, Juni 2, 2025 katika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, ambapo aliwasilisha kwa hawariri hao taarifa kuhusu safari ya Mageuzi, Mafanikio, Mikakati na Muelekeo wa taasisi na mashirika y umma nchini.
Jun 5, 2025
Home
featured
Uchumi
MIKAKATI YA MSAJILI WA HAZINA KUIMARISHA MASHIRIKA KUENDANA PIA NA ILANI YA CCM YA 2025/30
MIKAKATI YA MSAJILI WA HAZINA KUIMARISHA MASHIRIKA KUENDANA PIA NA ILANI YA CCM YA 2025/30
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇