RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi mbalimbali ikiwemo kumteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Lazaro Jacob Twange kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Taarifa ya leo Mei 06 iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa Rais Samia amemhamisha Mhe. Albert Gasper Msando kutoka Wilaya ya Handeni kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuchukua nafasi ya Lazaro Jacob Twange .
Rais Samia amemhamisha Mhe. Japhari Mghamba Kubecha kutoka Wilaya ya Tanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni huku akimhamisha Mhe. Dadi Horace Kolimba kutoka Wilaya ya Karatu kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga.
Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu, Lameck Karanga Nganga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu huku Bahati Migiri Mfungo ambaye alikuwa Afisa Tarafa ya Mbuguni, Wilayani Arumeru akiteuliwa ku wa Katibu Tawala wa Wilaya ya Karatu.
Vilevile Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Andrew William Massawe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA). Bw. Massawe anachukua nafasi ya Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman ambaye amemaliza muda wake.
May 7, 2025
Home
featuread
Kitaifa
RAIS DK. SAMIA AMTEUA ALIYEKUWA DC UBUNGO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA TANESCGO
RAIS DK. SAMIA AMTEUA ALIYEKUWA DC UBUNGO KUWA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA TANESCGO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇