Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimetangaza kuwa Mkutano wake Mkuu wa saba utakafanyika kwa siku mbili kuanzia Mei 28, 2025 Jijini Dodoma ambao utaambatana na uchaguzi wa viongozi kwa nafasi mbalimbali kwa ngazi ya taifa, ikiwa ni baada ya kukamilika kwa chaguzi zilizokuwa zikiendelea nchini kote kwa ngazi za shule (Tawi), Wilaya na Mikoa.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CWT imesema, miongoni mwa nafasi za kitaifa zinazotarajiwa kufanyiwa uchaguzi ni pamoja na rais, Makamu wa rais, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mweka Hazina, Mwakilishi wa Walimu wenye ulemavu, Mwakilishi wa walimu vijana, Mwakilishi wa Walimu wanawake, Mjumbe wa kamati ya utendaji TUCTA kutoka CWT, Wadhamini watatu na Vitengo
mbalimbali vya chama.
"Chama kinawakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu kushiriki tukio lao hilo muhimu na la kihistoria. Aidha orodha ya wagombea wa nafasi imetolewa kwa Umma", imesema taarifa hiyo.
Your Ad Spot
May 21, 2025
Home
Elimu
featured
CWT KUFANYA UCHAGUZI MKUU MWISHONI MWA MWEZI HUU JIJINI DODOMA, 18 WAJITOKEZA KUWANIA URAIS
CWT KUFANYA UCHAGUZI MKUU MWISHONI MWA MWEZI HUU JIJINI DODOMA, 18 WAJITOKEZA KUWANIA URAIS
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇