Apr 8, 2025

TUTAKUWA BEGA KWA BEGA NA WAZIRI BASHE KULIOKOA ZAO LA CHAI- MWANYIKA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Kilimo, ambaye pia ni Mbunge wa Njombr, Deodatus Mwanyika amempongeza Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kazi kubwa kwa kuifanyia mabadiliko makubwa sekta ya kilimo nchini ikiwemo kuchukua maamuzi magumu kwa lengo la kuhakikisha kilimo kinasonga mbele.

Amesema kuwa Katamati hiyo ya Bunge itaendelea kuwa bega kwa bega na yeye kuiuna zao la chai ambalo hivi sasa linadorora na kwamba hiyo kazi itakuwa ya kufa na kupona. Aidha amewajia juu wawekezaji wakubwa wanaodidimiza zao hilo tegemeo la wananchi wa hali ya chini na kwamba hatosita kuwaita kuwa ni wahujumu uchumi. Ameyasema hayo wakati wa Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Zao la Chai uliofanyika kwenye Hoteli ya Morena jijini Dodoma Aprili 8, 2025, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Hussein Bashe.


Mwanyika akijadiliana jambo na Waziri Bashe.

Waziri Bashe akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Chai Tanzania, Abdulmajid Nsekela akiongoza mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu akielezea changamoto wanazokumbana nazo wakulima wa chai ikiwemo ya kutolipwa malipo yao ya chai kwa muda wa miezi mitatu sasa.


Wadau wa Tasnia hiyo wakiwa katika mkutano huo.






IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages