Apr 13, 2025

RAIS DK. SAMIA AOMBOLEZA VIFO VYA MKURUGENZI MTENDAJI TANESCO NA DEREVA

Rais wa Jamhusri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, ameomboleza vifo vya vifo vya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, vilivyotokea usiku wa kuamkia leo Aprili 13, 2025, kwa ajali ya barabarani eneo la Bunda, Mkoa wa Mara.

 

 "Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya vifo vya Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), pamoja na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, vilivyotokea usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya barabarani eneo la Bunda, Mkoa wa Mara.


Natoa pole kwa familia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko, watumishi wa TANESCO, ndugu jamaa na marafiki.


Namuomba Mwenyezi Mungu azijaalie familia, ndugu, jamaa na marafiki subra, uvumilivu na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu.


Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Amina", imesema Taarifa ya Ikulu.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages