Dkt. Evance Chande amesimikwa rasmi kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Karmeli Assembilies of God (KAG) katika sherehe zilizofanyika Makao Makuu ya kanisa hilo Ipagala jijini Dodoma Aprili 19, 2025. Hivi sasa kanisa hilo lina matawi 35 nchini.
Mgeni rasmi katika sherehe hizo alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye hata hivyo aliwakilishwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Sherehe hizo zilizofana zilihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa vyama, serikali, wachungaji na maaskofu akiwemo Askofu Dkt. Namsasi aliyechukua jukumu la kumsimika uaskofu mkuu Dkt. Chande.
Sherehe hizo zilizotawaliwa na shangwe na vigelegele kutoka kwa waumini wa kanisa hilo na wageni waalikwa zilihanikizwa na nyimbo za injili kutoka kwa kwaya za kanisa hilo ikiwemo kwaya ya watoto.
Dkt. Chande akivishwa kola ya uaskofu.
Akikabidhiwa cheti mbele ya mke wake Joyce.Dkt. Chande akitia saini kwenye cheti cha uaskofu.
Akiombewa wakati wa kusimikwa uaskofu.
Akipongwezwa na Askofu Namsasi.
Dkt. Chande akisalimiana na Waziri Anthony Mavunde.
Maandamano ya maaskofu na wachungaji wakiingia kanisani katika ibada maalumu ya kusimikwa Dkt. Chande.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇