KATIKA kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita,inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, biashara ya mbolea nchini imekua kwa kiasi kikubwa ambapo wafanyabiashara wa mbolea waliopewa leseni wameongezeka kutoka 3,069 mwaka 2020/21 hadi 7,302 Februari, 2025.
Aidha, upatikanaji wa
mbolea umeongezeka kutoka tani 766,024 mwaka 2020/2021 hadi tani 1,213,729
mwaka 2023/2024, uingizaji wa mbolea umeongezeka kutoka tani 504,122 mwaka 2020/2021
hadi tani 728,758 mwaka 2023/2024 na uzalishaji wa ndani umeongezeka kutoka
tani 42,695 mwaka 2020/2021 hadi tani 158,628 mwaka 2023/2024.
Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
Ametaja mafanikio mengine kuwa ni Kutokana na kuongezeka kwa viwanda
vya kuzalisha mbolea na visaidizi vya mbolea kutoka viwanda 16 mwaka 2020/2021
hadi viwanda 33 mwaka 2023/2024. Kati ya viwanda hivyo, vitatu (3) ni
vikubwa, viwanda 11 ni vya kati na
viwanda 19 ni vidogo.
"Taifa limeshuhudia ongezeko la matumizi ya mbolea kutoka tani 363,599 mwaka 2020/2021 hadi tani 840,714 mwaka 2023/2024. Ongezeko hilo limewezesha kuongezeka kwa matumizi ya mbolea kutoka kilo 19 za virutubisho kwa hekta mwaka 2020/2021 hadi kilo 24 za virutubisho kwa hekta mwaka 2024/2025
Lengo ni kufikia kilo 50 za virutubisho kwa hekta ifikapo
mwaka 2033 kwa kuzingatia makubaliano ya Wakuu wa Nchi za Afrika yaliyofanyika
Nairobi 2024,"amesema Laurent.
Amefafanua kuwa kuongezeka
kwa matumizi ya mbolea nchini kumechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 19,980,718 mwaka 2020/2021
hadi tani 22,803,316 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la asilimia 14 na kufanya
utoshelevu wa chakula nchini kufikia asilimia 128.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇