KUTOKANA na maboresho yanayoendelea na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali, mapato ya Bohari ya Dawa yameendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 315.1 kwa mwaka wa fedha 2021/22, hadi kufikia shilingi bilioni 553.1 kwa mwaka wa fedha 2023/24 ikiwa ni ongezeko la shilingi bilioni 238 ambayo ni sawa na asilimia 76.
Aidha,
katika kipindi cha Julai 2024 hadi Februari 2025, Bohari ya Dawa imepata mapato ya
thamani ya shilingi bilioni 400.2 sawa na asilimia 115 ya lengo la kusambaza bidhaa
za afya zenye thamani ya shilingi bilioni 346.6.
Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere Tukai alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa MSD katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita leo Machi 19, 2025, katika Ofisi za Idara ya Habari - MAELEZO, jijini Dodoma.
"Kutokana na kuimarika kwa utendaji wa Bohari ya Dawa, makusanyo ya fedha kutoka kwenye vituo vya kutolea
huduma za afya yameendelea kuongezeka katika kipindi cha Serikali cha awamu ya sita
ambapo makusanyo yameongezeka kutoka shilingi bilioni 54.2 mwaka 2021/2022
hadi kufikia shilingi bilioni 118.9 mwaka 2023/2024," amesema Tukai.
Aidha, makusanyo ya fedha katika miezi saba ya mwaka wa fedha 2024/25 yanakaribia
makusanyo ya mwaka mzima uliopita hivyo kuonesha kuimarika kwa upatikanaji wa
bidhaa za afya.
Tukai amefafanua kuwa, mwaka wa fedha 2022/23, makusanyo ya fedha hayakuongezeka
kwa kuwa MSD ilikuwa inahudumia fedha za wateja zilizokuwa kwenye akaunti za MSD.
Ametaja sababu za ongozeko hilo kuwa limetokana na maboresho yanayoendelea
yaliyowezesha kupatikana kwa bidhaa nyingi Bohari ya Dawa zinazoendana na mahitaji
ya vituo, kuongezeka kwa uwezo wa wateja kulipia bidhaa, kuimarika kwa mahusiano
kati ya MSD na wateja.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Bw. Mavere Tukai akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇