Mar 14, 2025

ZAIDI YA KAYA 6000 MASIKINI ZAUNGANISHIWA MAJI ARUSHA



 Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA),  Mhandisi Justine Rujomba amesema kuwa Mamlaka hiyo imewezesha zaidi ya kaya  masikini 6000 zimeunganishiwa maji kwa gharama nafuu ya sh. 30,000 kwa Kila kaya.

Pamoja na mambo mengine, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Machi 14, 2025, kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Mhandisi Rujomba amesema kuwa AUWSA imevunja  rekodi kwa kutoa huduma ya maji kwa asilimia 99 badala ya asilimia 95 inayotakiwa kufikiwa ifikapo 2025 kwa mujibu wa utekekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
MHARIRI
BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages