Mar 20, 2025

MWENEZI MALUGU WA CHIBE, SHINYANGA MJINI AMPONGEZA RAIS SAMIA

Dkt Dismas Lyassa na Vikta Makinda, Shinyanga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt Samia Suluhu Hassan anapongezwa kutokana na mikakati yake bora ya kuongoza nchi na chama kwa ujumla.


Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Chibe, Jimbo la Shinyanga Mjini mkoani Shinyanga, ndugu Daud Malugu (pichani) akizungumza na CCMchama Blog anasema Rais Samia amekifanyia heshima kubwa chama na Watanzania kwa ujumla wake.


"Kwa mfano katika chama tulikuwa tunapata shida usafiri, lakini sasa kila kata Tanzania imepewa usafiri  wa pikipiki jambo ambalo linarahisisha usafiri kwa kiasi kikubwa," anasema Malugu.


Malugu anasema pia kwamba katika suala la maendeleo karibu kila sekta imekuwa na maendeleo makubwa katika kata yake, Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.


"Kwa miaka mingi hapa Chibe tulikuwa na changamoto ya kutokuwa na daraja linalounganisha Chibe na Kata ya Old Shinyanga, ni Dkt Samia amewezesha daraja hilo kujengwa na hivyo kutuondolea adha ya usafiri hasa wakati wa masika, kwani maji yalikuwa yakijaa hapo mtoni na kusababisha watu kushindwa kupita," anasisitiza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages