Mar 14, 2025

MITAMBO 290 YA UCHUNGUZI YANUNULIWA AWAMU YA RAIS SAMIA - MKEMIA MKUU WA SERIKALI


 Mkemia Mkuu wa Mamlaka ya Maabara ya Serikali (MMS), Dkt. Fidelice Mafuniko ametaja moja ya mafanikio waliyopata katika kipindi miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan ikiwemo kwamba  ununuzi wa mitambo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma za uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara.

Amesema katika kipindi hicho, imenunuliwa mitambo mikubwa kumi na sita (16) na midogo 274 yenye thamani ya jumla ya Shilingi Bilioni 17.8 na kwamba ununuzi wa mitambo hiyo umeendelea kuimarisha uchunguzi wa kimaabara na kuendelea kutoa huduma bora za uchunguzi wa Kisayansi wa kimaabara kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.

Pamoja na mambo mengine, ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari -MAELEZO jijini Dodoma Machi 14, 2025, kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo kuelekea maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, akiendelea kutaja mafanikio, Dkt. Mafuniko amesema kuwa Mamlaka ilipokea na kuhudhuria wito wa Mahakama 6,986 kutoka mahakama mbalimbali nchini kwa ajili ya kutoa ushahidi wa kitaalamu. Utoaji wa ushahidi huo umechangia katika mnyororo wa Haki Jinai kwa kutoa/maamzi haki kwa mhusika na kwa wakati, hivyo kuchangia kuleta, amani na utulivu wa nchi. 



No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages