Mar 22, 2025

EWURA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeshiriki katika maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya Maji kitaifa, yaliyohitimishwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Machi 22, 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Mhe. Rais amesisitiza uvunaji wa maji ya mvua, utunzaji vyanzo vya maji kwa kulinda mazingira na miundombinu ya maji ili upatikanaji wa maji uwe wa uhakika, salama, na endelevu.

Wiki ya maji kitaifa, imeadhimishwa kuanzia tarehe 16-22 Machi, ikiwa na kauli mbiu , “Uhifadhi wa Uoto wa Asili kwa Uhakika wa Maji.”

 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kulia) na viongozi wengine wa EWURA, wakifuatilia kwa makini maadhimisho hayo.  

 Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile (kulia) na viongozi wengine wa EWURA, wakifuatilia kwa makini maadhimisho hayo.

Ofisa Udhibiti Ubora wa Maji, Bw. Noel Mirwatu, akitoa elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maji kwa mteja aliyetembelea banda la EWURA wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji, Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages