Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021, Mamlaka ya Maji Safui na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeendelea na utekelezaji wa miradi zaidi ya ishirini na tano (25) yenye thamani ya fedha za Kitanzania Sh. billioni 987.6.
Kati ya hizo Bilioni 987.6. Miradi yenye thamani ya Tsh Bilioni 232.9 imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi. Miradi yenye thamani ya Tsh Bilioni 754.7 bado ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Hayo yameelezwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi Mkama Bwire, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Machi 11, 2025 jijini Dodoma, kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, miradi iliyopo katika mipango ya muda mfupi na mrefu yenye thamani ya Tsh Trilioni 3.1 imebuniwa na iko katika hatua mbalimbali za maandalizi.
Mhandisi Bwire amefafanua kuwa, fedha hizo zinajumuisha gharama za usanifu, ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya uzalishaji,usafirishaji na usambazaji wa majisafi, pamoja na ujenzi, upanuzi na ukarabati wa miundombinu ya ukusanyaji, usafirishaji, upokeaji na uchakataji wa majitaka.
Miradi hiyo inatekelezwa kwa kutumia fedha za makusanyo ya DAWASA, Serikali kuu na mikopo ya
masharti nafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, wakiwemo Benki ya Dunia, Serikali ya Korea
Kusini (kupitia Benki ya Exim ya Korea) na Serikali ya India (kupitia Benki ya Exim ya India).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇