LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 17, 2025

RAIS SAMIA AMEWEZESHA ASILIMIA 90 YA BARABARA KUWA KATIKA HALI NZURI

Mkurugenzi wa Mipango ya miundombinu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi  amebainisha kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan hali ya barabara kuu na za mikoa imeendelea kuimarika ambapo barabara zilizopo katika hali nzuri na wastani zimekuwa karibu asilimia 90 ya jumla ya mtandao wote wa barabara wenye kilomita 37,225.72.


Mhandisi Mlavi ameyasema hayo mapema leo hii jijini Dodoma Februari 17,2025 katika mkutano na waandishi wa habari akielezea mafanikio na mwelekeo wa Tanroads kuelekea Maadhimisho ya Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya sita.


Ameongeza kuwa kilomita 2,031.11 za barabara zimeendelea kujengwa kwa kiwango cha lami,huku upembuzi yakinifu na usanifu wa barabara za kilomita 4,734.43 ukiendelea.


"Katika kipindi cha miaka minne ,hali ya barabara kuu na za mikoa imeendelea kuimarika ambapo barabara zilizo katika hali nzuri na wastani zimekuwa karibu 90% ya jumla ya mtandao wote wa barabara wenye kilomita 37,225.72".


"Barabara zenye urefu wa jumla ya kilimo 2,031.11 zimeendelea kujengwa kwankiwango cha lami,Aidha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara zenye jumla ya kilomita 4,734.43 na madaraja kumi unaendelea,"amesema Mlavi.

Aidha, Mhandisi Mlavi amesema kuwa jumla ya madaraja makubwa 9 yamekamilika kujengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 381.301 huku madaraja mengine kumi yatakayogharimu Bilioni 985.802 yakiwa yanaendelea na ujenzi, wakati madaraja mengine makubwa 19 yakiwa katika maandalizi ya kujengwa.


Mbali na hayo, pia amezungumzia suala la ujenzi wa barabara ya mzunguko iliyopo nje ya Jiji la Dodoma yenye urefu wa kilomita 112 ambapo hadi kufika Februari 2025 ujenzi umefikia asilimia 91 kwa sehemu ya kwanza  Nala,Veyula,Mtumba,Ihumwa Bandari kavu(KM52.3) na asimilia 85 kwa sehemu ya pili ya Ihumwa Bandari kavu, Matumbulu,Nala (KM 62).

Pia amesema Serikali imeweka mikakati ambayo  imependekezwa na kamati ili kuongeza ushiriki wa wazawa kwenye kazi za ujenzi kwa kutenga asilimia 10 ya bajeti ya kila mwaka ya maendeleo kwa asilimia 30 ya bajeti ya maendeleo kwa ajili ya upendeleo kwa Wazawa na kutenga angalau asilimia 5 ya bajeti ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya makundi maalum.


Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amezitaka Taasisi za Serikali kuwa na muitikio mzuri katika utoaji wa Taarifa ikwemo mafanikio ya Taasisi zao kupitia Mikutano hii inayoendelea kwani yapo mengi ambayo Serikali ya Awamu ya sita ndani ya miaka minne imeyafanya na Wananchi wanapaswa kuyajua kupitia vyombo vya habari.

Wakala wa Barabara Tanzania ilianzishwa mwaka 2000 kwa lengo la usimamizi wa ujenzi,ukarabati na matengenezo ya barabara na madaraja katika barabara za Kitaifa na ujenzi wa viwanja vya ndege.


Mkurugenzi wa Mipango ya miundombinu Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Ephatar Mlavi  
katika mkutano na waandishi wa habari akielezea mafanikio na mwelekeo wa Tanroads kuelekea Maadhimisho ya Miaka 4 ya Serikali ya awamu ya sita.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akisema maneno ya utangulizi kabla ya kumkaribisha Mhandisi Mlavi kuzungumza na vyombo vya habari.




No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages