Na Victor Makinda. Morogoro
Mjumbe wa Halmashhauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM, Mkoa wa Morogoro, Jonas Nkya, amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuwa kiongozi msikivu na mnyeyekevu kwa wananchi wake huku akitia bidii, juhudi na marifa kuwakwamua katika lindi la umaskini.
Nkya ameyasema hayo ofisini kwake mjini Morogoro wakati alipokuwa akizungumza na CCM Digital alipokuwa akitoa maoni yake kuhusu miaka minne ya Rais Samia Madarakani.
"Zimebaki siku chache, takribani mwezi mmoja Rais Samia atimize miaka minne tangu aingie madarakanj, kwangu mimi pamoja na hatua kubwa za maendeleo ambazo Rais Samia amewaletea wananchi wa Tanzania, lakini ninaona namna ambavyo Rais Samia amebaki kuwa ni yule yule, mwenye upendo na unyenyekevu kwa wananchi wake."
Akifafanua amesema kuwa baadhi ya viongozi wa ki-Africa huingia madarakani wakiwa wanyenyekevu kwa wananchi wao, lakini baadae hugeuka na kuwa watu dharimu wasiojali maslahi ya wanananchi wanao waongoza.
"Rais Samia amebaki kuwa ni kiongozi mnyenyekevu, msikivu na anayeguswa na matatizo ya wananchi wake huku akipambana kuwaletea ustawi wa kweli."
Ameongeza kusema kuwa utekelezwaji wa miradi mikubwa ya maendeleo kwenye sekta za elimu, afya, maji, umeme na miundombinu ni kielelezo cha namna uongozi wa Rais Samia unajali maslahi ya wananchi.
" Maendeleo ambayo nchi imeyafikia katika kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais Samia ni makubwa yasiyo mfanowe, hii inadhihirisha jinsi Rais wetu anavyo simamia kwa uaminifu kodi na rasilimali zetu kwa ajili ya maendeleo yetu." Amesema Nkya.
Akizungumzia amani na utulivu nchini, Nkya amesema kuwa uongozi wa Rais Samia umeimarisha amani, utulivu udugu na umoja wa kitaifa.
" Nchi yetu ipo salama, tuna amani ya kutosha, tumeendelea kuwa wamoja na Muungano wetu umezidi kuwa imara, haya ni matunda ya uongozi thabiti wa Rais Samia unaojali maslahi ya Taifa. Amesema.
Amesema kuwa R4 za Rais Samia ni kielelezo kingine kuwa Rais Samia amejithatiti kuitunza amani yetu na umoja wa kitaifa.
Nkya anawaasa Watanzania kuendelea kuchapa kazi kwa bidii ili Taifa lizidi kusonga mbele.
Amewataka watanzania kuendelea kuitunza amani hususani kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
" tuwakatae wale wote ambao sera zao ni za vurugu zinazoweza kuhatarisha amani yetu, tuwaunge mkono na kuwachagua wale wanaoitunza amani yetu." Amesema.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇