Mombasa, Kenya
Timu nne za Bunge la Tanzania zimeshuka dimbani leo katika mashindano ya Michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuibuka kidedea katika michezo mitatu.
Timu zilizocheza katika mashindano hayo yanayoendelea Jijini Mombasa nchini Kenya ni timu ya Mpira wa Miguu, timu ya Mpira wa Pete na timu ya Mpira wa Kikapu wanawake na wanaume.
Katika mpira wa pete timu ya Bunge la Tanzania iliichakaza timu ya Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kwa magoli 50-2, viana wa ufungaji wakiwa Mheshimiwa Dk. Christina Mzava, Mheshimiwa Esther Matiko na Mheshimiwa Ngwasi Kamani.
Upande wa kikapu Wanaume, timu ya Tanzania imejichukulia pointi za mezani baada ya wapinzani wao timu ya Bunge la Sudani ya Kusini kushindwa kufika uwanjani, huku upande wa soka timu ya Bunge la Tanzania ikitoka sare ya bao 1-1 na timu ya ya Bunge la Burundi, goli pekee la Tanzania likifungwa na Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki katika kipindi cha kwanza cha machezo huo.
Kesho timu za Tanzania zitakazoingia ulingoni ni za Gofu, Mpira wa Pete na mchezo wa kuvuka kamba Wanaume na Wanawake.
Wachezaji wa Timu ya Bunge ya Mpira wa Pete wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge la Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mheshimiwa Joseph Ntakirutimana kabla ya kuanza kwa mchezo na Timu ya Bunge la EALA. Mchezo huo uliofanyika katika Uwanja wa Aghakani Jijini Mombasa, Kenya, ulimalizika kwa Timu ya Tanzania kuifunga Timu ya EALA mabao 50-2.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇