MTANZANIA Mkali wa Mbio Ndefu, Alphonce Felix Simbu, ameshika nafasi ya nne akikimbia kwa muda wa saa 2, dakika 4 na sekunde 38 (2:04:38 PB), kwenye mbio za Valencia Marathon 2024, zilizofanyika mapema leo huko Valencia nchini Hispania.
Licha ya kushuka nafasi ya nne, huo ni muda bora zaidi kwa Simbu mwenyewe, akizidiwa sekunde 14 tu Mkenya Daniel Mateko, aliyeshika nafasi ya tatu kwa kutumia saa 2, dakika nne na sekunde 24 (2:04:24) na kutwaa medali ya shaba.
Mwanariadha wa Ethiopia, Dress Geleta alishika nafasi ya pili baada ya kutumia saa 2 dakika mbili na sekunde 38 (2:02:38), huku Mkenya Sebastian Sawe akiibuka kinara kwa kukimbia kwa saa 2 dakika 2 na sekunde tano (2:02:05) na kutwaa medali ya Dhahabu.
Matokeo hayo, yanakuja wiki moja tu tangu Simbu na Magdalena Crispine Shauri walishinda Medali za Dhahabu kwa muda wa 2:17:19 na 2:36.29 kwenye Mashindano ya Majeshi Afrika (AMGA 2024) yaliyofanyika huko Abuja , Nigeria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇