LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 13, 2024

EWURA YAHAMASISHA UVUNAJI WA MAJI YA MVUA NA MATUMIZI YA NISHATI SAFI

 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo Tar.13 Desemba 2024, imefanya mafunzo kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) jijini Dar es Salaam, huku msisitizo ukiwa kwenye uvunaji wa maji ya mvua katika kukabiliana na upungufu wa huduma za maji katika maeneo mbalimbali.

Pia katika mafunzo hayo mkazo umetolewa katika kuhamasisha matumizi ya Nishati safi ya kupikia na kwenye magari.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, Dkt. James Andilile, alisema lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo wanahabari kutoa taarifa za sekta ya nishati na maji kwa usahihi na kwa wakati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Pamoja na uhamasishaji wa uvunaji maji ya mvua na matumizi ya nishati safi, mafunzo hayo pia yalijikita katika historia ya EWURA, shughuli za udhibiti wa sekta za umeme, petroli, gesi asilia na maji pamoja na mafanikio ya udhibiti tangu kuanzishwa kwa EWURA mwaka 2006.

Naye Katibu wa JOWUTA Bw. Suleiman Msuya aliishukuru EWURA kwa mafunzo hayo huku akitoa rai kwa waandishi wa habari kutumia elimu walioipata kutoa taarifa za nishati na maji kwa usahihi zaidi.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano EWURA, Bw.Titus Kaguo, akitoa mafunzo ya elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maji,uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya nishati safi kwa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA) leo Disemba 13,2024.

Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki EWURA, Mhandisi. Mwanamkuu Kanizio, akijibu swali kuhusu sekta ya umeme wakati wa mafunzo hayo.

    

Baadhi ya waandishi wa habari wanachama wa JOWUTA, wakifatilia kwa makini mafunzo hayo leo.

  

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo, aliyekaa katikati,akiwa katika  picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa JOWUTA mara baada ya kumalizika kwa  mafunzo ya elimu ya udhibiti wa huduma za nishati na maj,uvunaji wa maji ya mvua na matumizi ya nishati safi kwa Wanachama hao  leo Disemba 13,2024.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages