LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2024

DKT NCHIMBI ASHIRIKI KUAGA MWILI WA MAREHEMU DKT. NDUGULILE

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi akitoa salamu za rambirambi za chama.aliposhiriki kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika ka Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mhe. Faustine Engelbert Ndugulile, leo Jumatatu, tarehe 2 Desemba 2024, katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na baadhi ya waombolezaji aliposhiriki kutoa heshima za mwisho na kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika ka Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mhe. Faustine Engelbert Ndugulile, leo Jumatatu, tarehe 2 Desemba 2024, katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar Es Salaam.


Wapambe wa Bunge wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa marehemu Dkt. Ndugulile.

Dkt. Nchimbi  akizungumza jambo na baadhi viongozi walioshiriki kuuaga mwili wa marehemu, Dkt. Ndugulile.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Samia  Suluhu Hassan akiwa na baadhi ya viongozi akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Dkt Nchimbi.






No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages